SiasaMarekani ya Kusini
Cuba yaanza kuwaachia maelfu ya wafungwa
4 Aprili 2026
Matangazo
Zaidi ya wafungwa 20 waliachiliwa kutoka gereza la La Lima mashariki mwa Havana, wakiwa wameshikilia nyaraka zao za kuwa huru, wakilia na kuwakumbatia jamaa zao ambao walikuwa wakiwasubiri tangu asubuhi.
Haijajulikana hadi sasa ikiwa wale walioachiliwa Ijumaa ni wafungwa wa kisiasa, kwani hakuna orodha iliyochapishwa. Mamlaka za Cuba zinakana kuwashikilia wafungwa wa aina hiyo.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema inafahamu taarifa kuhusu kuachiliwa kwa wafungwa, lakini ikaongeza kuwa haijulikani wazi kama wafungwa wowote wa kisiasa watakuwa miongoni mwao.