1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Congo : ongezeko la maambukizi ya Covid-19 mjini Goma

19 Agosti 2021

Wakaazi wa mji wa Goma mashariki mwa Congo wakumbwa na wasiwasi kufuatia ongezeko la vifo kutokana na ugonjwa wa Covid-19, huku kukiwa na uhaba wa chanjo.

https://p.dw.com/p/3zBfh
DR Kongo Covid-19 Impfung
Picha: Olivia Acland

Hapa ni  katika shamba la makaburi Makao mbali kidogo na mji wa Goma ,eneo ambako mamia ya watu huwasili  kila siku ili kuwazika wapendwa wao walioaga dunia. Tangu kutangazwa kwa wimbi la tatu la virusi vya corona hapa nchini congo kunashuhudiwa hivi sasa ongezeko kubwa la vifo tofauti na mwaka mmoja uliopita ,toka watu wa 5 hadi kufikia 20 kwa siku kama anavyo shuhudia mkaazi huyu  anaye ishi kandoni mwa shamba hili la makaburi. 

Wadadisi wa maswala ya afya  hapa kivu ya kaskazini wanahusisha vifo hivi nakuto heshimu kanuni za afya lakini pia ukaidi wa maagizo ya kuvaa barakoa kwa baadhi ya wananchi wa Goma kumekuwa ni tishio kubwa .

Hata hivyo, mwenyekiti wa mashirika ya kiraia  mjini Goma Mario Ngavo, amewataka wananchi kuwa na mwelekeo wa pamoja katika juhudi za kupambana dhidi ya janga hili la corona. 

Uhaba wa chanjo

Kongo: Erneuter Ausbruch von Ebola
Picha: picture-alliance/AP/S. Mednick

Kufuatia ongezeko la visa vipya vya virusi vya corana, baadhi ya hospitali na vituo vya afya vimekuwa na uwezo mdogo wakuwashughulikia wa gonjwa wanao wasili kwa ajili ya matibabu.

Mapema mwanzoni mwa juma hili, idara ya afya hapa nchini imewasilisha kiwango cha dozi 4300 zitakazotolewa kwa wale walio pata dozi ya kwanza ya chanjo ya aina Astrazenecca ,chanjo ambayo bado inaendelea kupingwa na baadhi ya wakaazi hapa nchini jamuhuri yakidemokrasi ya congo kufuatia habari za upotoshaji zinazo sambazwa mitanadaoni.

Hata hivyo kulingana na takwimu kutoka idara ya afya hapa kivu ya kaskazini  inakadiriwa kuwa tangu mwezi wa Mei hadi Julai 10 watu 6,775 walipewa dozi ya kwanza  chanjo dhidi ya virusi vya corona.