Colombo.Machafuko yazuka upya nchini Sri Lanka. | Habari za Ulimwengu | DW | 09.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Colombo.Machafuko yazuka upya nchini Sri Lanka.

Kumeripotiwa machafuko nchini Sri Lanka siku moja baada ya kiasi cha Watamil 45 kuuwawa na wengine 125 kujeruhiwa kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na vikosi vya jeshi la Serikali, katika jimbo linaloshikiliwa na waasi wa Kitamil, mashariki mwa nchi hiyo.

Katika tukio la hivi punde mwanajeshi mmoja ameuwawa na wengine wawili wamejeruhiwa, wakati waasi wa Kitamil walipokishambulia kituo cha kijeshi kaskazini mwa Jaffna.

Kundi la waangalizi wa kimataifa wanaosimamia makubaliano ya kuweka chini silaha ya mwaka 2002 wameanza kulichunguza tukio la hapo jana.

Zaidi ya raia 1,000 wameshauliwa mwaka huu kutokana na mapigano ya pande hizo mbili.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com