COLOMBO: Watu 29 wauawa katika mapigano mapya Sri Lanka | Habari za Ulimwengu | DW | 15.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

COLOMBO: Watu 29 wauawa katika mapigano mapya Sri Lanka

Watu wapatao 30 wameuawa kutokana na mapigano mapya katika peninsula ya Jaffna nchini Sri Lanka.

Wizara ya ulinzi ya nchi hiyo imesema kuwa wanajeshi wawili waliuawa kwa bomu lililotegwa njiani.

Wizara hiyo inatuhumu kuwa wapiganaji wa kitamil walitega bomu hilo.

Watu zaidi ya alfu 5 na mia nne wameshauawa nchini Sri Lanka kutokana na mipigano katika kipindi cha miezi 21 iliyopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com