1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Coco Gauff amshangaza Venus Williams tena

20 Januari 2020

Mashindano ya Tennis ya Australian Open yanaendelea huko Australia. Hapo Jumapili majina makubwa katika mchezo huo yalifuzu kwenye raundi ya pili. Naomi Osaka ambaye ndiye bingwa mtetezi upande wa kina dada alifuzu.

https://p.dw.com/p/3WU4x
Tennis Spielerin Cori Gauff USA
Picha: picture-alliance/empics/M. Egerton

Naomi akafuatwa na Serena Williams na bingwa mtetezi upande wa kina kaka Roger Federer, wote hao wakijikatia tiketi ya raundi ya pili.

Aliyewashangaza wengi kwa mara nyengine tena ni mwanadada kutoka Marekani mwenye umri wa miaka kumi na tano Coco Gauff ambaye kwa mara nyengine tena alimbandua Venus Williams, kama alivyofanya mwaka jana katika Wimbledon na kupelekea ulimwengu kumtambua. Huyu hapa Gauff akizungumza baada ya mechi hiyo.

"Nataka niseme asanteni sana. Mulikuwa munaliimba jina langu na nilifikiri hilo litafanyika katika mashindano ya US Open pekee, kwa hiyo nyinyi kufanya hivyo hapa Australia ni jambo linalonipa faraja sana," alisema Gauff.