1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chelsea yakaribia kutwaa ubingwa Uingereza

13 Aprili 2015

Chelsea iko pointi saba mbele katika msimamo wa ligi ya Uingereza Premier League baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Queens Park Rangers. Vijana hao wa kocha Jose Mourinho wanakaribia kutwaa ubingwa

https://p.dw.com/p/1F7DC
Champions League Achtelfinale Paris St. Germain FC Chelsea
Picha: Franck Fife/AFP/Getty Images

Lakini habari ya mjini ilikuwa kipigo cha mabao 4-2 ilichotoa Manchester United dhidi ya Manchester City, "The noisy Neghbours" kama wanavyotambuliwa na majirani zao , watani wa jadi Manchester United.

Kocha mkuu wa Manchester City Manuel Pellegrini amekataa kuzungumzia hali yake ya baadaye baada ya kisago hicho hali inayofuta matumaini ya timu hiyo kutetea ubingwa wake.

Kipigo cha nne mfululizo ugenini kimekiacha kikosi hicho cha Manuel Pellegrini kikiwa nafasi ya nne, pointi 12 nyuma ya viongozi Chelsea, wakati Liverpool inaweza kupunguza mwanya uliopo hadi pointi nne iwapo itaishinda NewCastle usiku wa leo.

Pellegrini amekubali jukumu la kipigo hicho , akisema njia pekee tunayoweza kubadilisha hali hii ni kushinda."

Lakini raia huyo wa Chile , ambaye huenda ni kocha mwingine wa premier League kibarua kuota majani , amesema: " Sitazungumzia kuhusu nafasi yangu. Sio muhimu."

Man United imesogea hadi nafasi ya tatu pointi moja nyuma ya Arsenal ambayo imeshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Burnley siku ya Jumamosi.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / dpae / rtre / afpe
Mhariri: Yusuf, Saumu