Chelsea yaifurusha Real Madrid 2 - 0 na kutinga fainali | Michezo | DW | 06.05.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Chelsea yaifurusha Real Madrid 2 - 0 na kutinga fainali

Chelsea imejikatia tiketi ya kucheza dhidi ya Manchester City katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayovikutanisha vilabu viwili vya England. Iliifunga Real Madrid jumla ya mabao 3 - 1 katika mikondo yote miwili

Mabao ya Timo Werner na Mason Mount yalihitimisha kibarua cha mkondo wa pili wa nusu fainali dhidi ya Real Madrid mjini London. Chelsea ilifuzu kwa jumla ya mabao matatu kwa moja kufutia sare ya 1 - 1 katika mkondo wa kwanza. Kocha Mjerumani Thomas Tuchel anarejea katika fainali baada ya kupoteza msimu uliopita akiwa na Paris Saint-Germain dhidi ya Bayern Munich.

Sasa Chelsea watakamatana na City yake Pep Guardiola mjini Istanbul mnamo Mei 29. Chelsea tayari iliiondoa Man City katika nusu fainali ya Kombe la FA Uingereza.