1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Matumaini ya Chelsea kupata nafasi mbili za juu ni ndoto

Deo Kaji Makomba
2 Julai 2020

Frank Lampard amekiri dhahiri shahiri kwamba timu yake ina safari ndefu ikiwa inataka kufanana na mwenendo uliooneshwa na timu za Liverpool na Manchester City katika kipindi cha misimu michache iliyopita. 

https://p.dw.com/p/3egFX
Großbritannien Fußball | Frank Lampard, Trainer Derby County
Kocha wa timu ya soka ya Chelsea, Frank LampardPicha: Reuters/Action Images/T. O'Brien

Huko nchini England kocha mkuu wa timu ya soka ya Chelsea Frank Lampard amekiri dhahiri shahiri ya kwamba timu yake ina safari ndefu ikiwa inataka kufanana na mwenendo uliooneshwa na timu za Liverpool na Manchester City katika kipindi cha misimu michache iliyopita. 

Kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa West Ham Jumatano iliyopita imeigharimu timu hiyo na kushindwa kuchupa juu ya Leicester kunako nafasi ya tatu na kwa sasa wako katika vita vya mbwa kupambana kuingia katika nafasi nne bora za juu.

"Ni kitu ambacho kimetokea mara chache msimu huu, tulikuwa na nafasi kuweza kupunguza pengo au kuruka juu ya timu," Lampard aliwaambia waandishi wa habari.

"Hiyo ni ishara ya mahali tulipo, tuna kazi ngumu sana ya kufanya kuweza kufikia mahali tunapotaka kuwa na hiyo ni sababu na miongoni mwetu tunaikimbiza Liverpool na Manchester City, kwa sababu ya msimamo wao wameendelea kwa wakati.

"Tunapaswa kutambua nafasi tuliyopo, tupo katika suala la kupigania nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa na kusonga mbele."

Lakini Lampard alisema kuwa ushindi ulihitaji kuwekwa katika mtizamo, na nafasi nne za juu bado ziko wazi.

Chanzo: dpa