Chelsea, City na Liverpool zawania ubingwa England | Michezo | DW | 28.03.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Chelsea, City na Liverpool zawania ubingwa England

Manchester City watajaribu kuwauwa ndege wawili kwa kutumia jiwe moja, wakati watakapojaribu wikendi hii kuwaongezea joto viongozi wa ligi Chelsea na pia kuyauwa matumaini ya Arsenal kutwaa ubingwa.

Ushindi wa City wa magoli matatu kwa sifuri dhidi ya Manchester United uliwaongeza karibu na Chelsea kwa pengo la points tatu huku wakiwa na mechi mbili za kucheza. Arsenal wako nyuma ya vijana wa Pelkegrini wakiwa na pengo la points tatu, lakini wamecheza mechi mbili zaidi na hawatataka kushindwa wakati timu hizo mbili zitakapokutana leo uwanjani Emirates.

Huku Liverpool wakisubiri hadi kesho Jumapili, wakati watakapowaalika nambari sita Tottenham Hotspurs, Cheslea watakuwa na fursa ya kupanua uongozi wao na points nne wakati watakapocheza ugenini dhidi ya Crystal Palace leo Jumamosi.

La liga

Nchini Uhispania ambapo pia kinyang‘anyiro cha taji kimepamba moto..Atletico Madrid wanakabiliwa na kibarua kigumu ugenini dhidi ya Athletic Bilbao leo Jumamosi katika juhudi zao za kutaka kusalia juu ya miamba Barcelona na Real Madrid.

Mara ya mwisho ambapo timu ambayo siyo Barcelona au Real Madrid imewahi kushinda La liga ni mwaka wa 2004 wakati Rafa Benitez aliwaongoza Valencia kutwaa uchampion. Na ni mwaka wa 2008 ambapo timu tofauti iliweza kumaliza msimu katika nafasi ya pili, na timu hiyo ilikuwa Villareal yake Manuel Pellegrini kwa wakati huo. Atletico wako mbele ya Barca na faida ya point moja na tatu mbele ya Real, wakati kukisalia mechi nane msimu kukamilika.

Barcelona pia watakuwa leo na mchuano mkali wa ugenini dhidi ya Espanyol. Real Madrid wanacheza leo dhidi ya mahasimu wao wa nyumbani Rayo Vallecano.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu