Charlie nani? Mwendesha baiskeli mwanafunzi ashinda dhahabu Madola | Michezo | DW | 07.04.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Charlie nani? Mwendesha baiskeli mwanafunzi ashinda dhahabu Madola

Si hata mashabiki wa mbio za baiskeli waliwahi kumsikia Charlie Tanfield mwaka mmoja uliopita, lakini sasa Mwingereza huyo kijana ni bingwa wa michezo ya Jumuiya ya Madola, akiweka rekodi ya muda mrefu.

Australien 2018 Commonwealth Games 2018 | Charlie Tanfield (Reuters/P. Childs)

Charlie Tanfield akisherehekea baada ya ushindi katika mbio za mwendeshaji mmoja mmoja za mita 4000 huko Anna Meares velodrome - Gold Coast, Australia, Aprili 6, 2018.

Kimsingi mwanafunzi huyo anaesomea uhandisi wa umekanika, ambaye bado ni mwanagenzi, kwa namna fulani alikwepa nadhari ya wakuu wa chama cha waendesha baiskeli cha Uingereza hadi hivi karibuni -- lakini hawezi kupuuzwa tena.

Tanfield alipata ushindi katika fainali ya mbio za mita 4,000 katika uwanja wa Anna Meares Veladrome mjini Brisbane siku ya Ijumaa, na kuongeza medali ya dhahabu juu ya ile ya fedha alioipta saa 24 kabla ya hapo.

Wakati akija katika michezo hiyo, Tanfield alisema kwa ujasiri kwamba alikuwa anafukuzia rekodi ya dunia ya saa 4:10.534 iliowekwa na raia wa Australia Jack Bobridge mwaka 2011.

Australien 2018 Commonwealth Games 2018 | Charlie Tanfield (Reuters/P. Childs)

Charlie Tanfield akipeperusha bendera ya taifa lake baada ya ushindi wa kushangaza.

Hakufanikiwa kuivunja rekodi hiyo, lakini bado aliweza kushinda katika moja ya muda mfupi zaidi katika historia ya michezo ya Jumuiya ya Madola, kwa muda wake wa  saa 4:11.455. Hakubahatisha.

Mwanzo wake

Tanfield alijitambulisha kwa hadhira kubwa zaidi wiki chache tu zilizopita wakati aliposhirikia kwa mara ya kwanza katika mashindano ya bingwa wa dunia ya UCI mjini Apeldoorn, Uholanzi.

Alikuwa sehemu ya timu iliyoshinda na alikosa kidogo kupata nafasi ya kupanda jukwaa la washindi kwa kuibuka wa nne katika mashindano ya mtu mmoja mmoja.

Tanfield alieanza kushiriki mchezo huo kikamilifu miezi miwili iliopita, kwa kusimamisha masomo yake ya chuo kikuu, anasema anafurahia "mambo yasio ya kawaida" katika mchezo huo kutokana na historia yake ya uhandisi wa umekanika. Lakini itakuwa kuongeza chumvi kusema kwamba daima alitegemewa kushinda medali.

Akiwa kijana, alipoteza hamasa ya mchezo huo, kabla ya kurejesha mapenzi yake kwake, lakini ulikuwa uundwaji wa timu yake ya KGF uliosadia kumfikisha alipo sasa hivi.

Australien 2018 Commonwealth Games 2018 | Charlie Tanfield (Reuters/P. Childs)

Charlie Tanfield (katikati) akionyesha medali yake ya dhabau alioshinda. Wengine ni mshindi wa medali ya fedha John Archibald wa Scotland, na wa tatu ni Dylan Kenneth wa New zealand alieshinda medali ya shaba.

Mafanikio ya kushangaza ya KGF -- ambao hawana ufadhili mkubwa ikilinganishwa na timu kubwa katika programu ya baiskeli ya Uingereza -- yalikuwa moja ya simulizi za mbio za baiskeli mwaka 2017 na ulivuta nadhari ya wakubwa katika mchezo huo nchini Uingereza.     

Baada ya kufanya mazoezi kwa muda wa miezi miwili, timu hiyo ya wanagenzi isiyo na fedha nyingi ilifanya vizuri katika mashindano ya ubingwa ya Uingereza mwaka huo.

Walibeba mafanikio hayo mjini Minski Januari mwaka huu, wakati Tanfield aliposhinda dhahabu ya kombe la dunia kwa mtu mmoja mmoja, na pia walishinda medali ya dhahabu kwa ngazi ya timu.

Mashujaa wao sasa wanatengezea filamu. "Matokeo yanazidi kuja na ni vizuri kuzidi kujidhihirisha mwenyewe katika jukwaa la kimataifa," alisema Tanfield.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/Afp.

Mhariri: Yusra Buwayhid

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com