Changamoto kileleni:Bundesliga: | Michezo | DW | 16.10.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Changamoto kileleni:Bundesliga:

Leverkusen yaumana na Hamburg

Bruno Labbadia (kocha wa Hamburg)

Bruno Labbadia (kocha wa Hamburg)

-Baada ya kinyanganyiro cha kati ya wiki hii cha kuania kufuzu kwa kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika Kusini,Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalio ya Kombe la Dunia, Danny Jordaan,afurahia kuona Argentina na Lionel Messi, wamekata mwishoe, tiketi yao ya Afrika Kusini-

-Nigeria na Tunisia ,zinabidi kusubiri hadi mpambano w mwisho.

-Mabingwa wa dunia-Itali na mabingwa mara 3 Ujerumani zimekata nazo tiketi zao za kombe la dunia bila kushindwa hata mara moja.

BUNDESLIGA:

Macho ya mashabiki wa Bundesliga, yanakodolewa leo mpambano kati ya timu 2 za kileleni:Bayer Leverkusen na Hamburg.Hizi ni timu 2 ambazo bado hazikushindwa tangu kuanza msimu huu.Isitoshe, kocha wa Hamburg,Bruno Labbadia,alikuwa kocha wa Bayer Leverkusen.Timu hizi mbili, zimepishana kwa magoli tu,Leverkusen ikishika usukani.

Katika Premier League-ligi ya Uingereza, Chelsea ina mtihani leo(Jumamosi) kuzima vishindo vya Aston Villa na kubakia kileleni.Mahasimu wao Manchester United,iliopo nafasi ya pili, wanacheza na Bolton Wanderes.Arsenal yaumana na Birmingham City.

Kwenye La Liga-Ligi ya Spian,mabingwa FC Barcelona bila ya jogoo lao Thiery Henry, lililoumia, wanapambana na Valencia.Barcelona yaongoza La Liga kwa pointi 3.Mahasimu wao Real madrid pamoja na Sevilla, wanafuata nafasi ya pili.

KOMBE LA DUNIA:

Kufuatia changamoto za kati ya wiki,Argentina ,mwishoe, imekuwa timu ya 4 kanda ya Amerika Kusini kuuwafata mahasimu na majirani zao Brazil; Chile na Paraguay katika kombe lijalo la dunia nchini Afrika Kusini.

Hatima ya Argentina na kocha wao Diego Maradona, ilikua haijulikani hadi dakika ya 84 ya mchezo, pale Mario Bolati, alipoitwa uwanjani na Maradona, kuliokoa jahazi lao lisiende mrama dhidi ya mabingwa w kwanza kabisa wa dunia -Uruguay.

Kuokoka kwa Argentina dakika ya mwisho,kumemfanya Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalio ya Kombe la Dunia, muafrika Kusini, Danny Jordaan, kuvuta pumzi na kufurahia kumuona stadi wa Barcelona, Lionel Messi atateremka uwanjani.

Sasa Jordaan, wasi wasi wake ni iwapo Ureno, itafuzu nayo kucheza kombe lijalo la dunia ili nyota nyngine ya dimba ulimwenguni -Cristiano Ronaldo, inawiri katika mawingu ya Afrika kusini. Kwani, Kombe lijalo la dunia bila ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, halitatimilia.

Tayri Afrika, imesha hakikishiwa mastadi wake 2 wa Afrika:Didier Drogba wa Ivory Coast na Michael Essien wa Ghana-timu mbili pamoja na wenyeji Afrika kusini,zilizokwisha kata tiketi zao za kombe la kwanza la dunia barani Afrika. Simba wa nyika -Samuel Eto-o, yuko njiani kuwafuata Johannesberg.

Jumla ya timu 23 kati ya zote 32, hadi sasa zimeshafuzu kwa kombe lijalo la dunia.Ni nafasi 9 tu zimesalia kujazwa: Katika Kanda ya Afrika, hadi sasa timu 2 zimefaulu:Ghana na Ivory Coast.

Kanda ya Ulaya, ni mabingwa wa dunia-Itali, mabingwa mara 3 wa dunia-Ujerumani,Holland,Serbia,Slovakia,Spain na Uswisi.

Eneo la Oceania ni Australia, Japan,Korea ya Kaskazini na Korea ya Kusini.Amerika ya kaskazini na ya kati: ni Marekani,Mexico na Hondurus.

Mabingwa wa Ulaya, Spian,wanapigiwa upatu mara hii kuwa ni wao watakao tawazwa mabingwa wa dunia.Hii inafuatia kuwa Spain , imeshinda mapambano yake 10 mfululizo na kupachika jumla ya mabao 28 .Ilikomewa mabao 5 tu langoni mwake.

Lakini si mabingwa wa Ulaya pekee wanaopigiwa upatu kutamba barani Afrika: Mabingwa wa dunia,Itali na hata Ujerumani, hawakushindwa pia katika kinyanganyiro cha cha kufuzu kwa Kombe la dunia 2010."Msingi wa kushinda Ujerumani kombe la Dunia 2010 ni imara kabisa"-alisema Joachim Loew,kocha wa Ujerumani.Lakini, ilikua kabla ya Ujerumani haikutoka sare dakika ya mwisho na Finland jumatano iliopita.

Marcello Lippi,kocha wa mabingwa wa dunia-Itali, ameshatoroka na Kombe jhilo Ujerumani 2006 na "mramba asali-harambi mara moja." Analitaka tena Kombe libaki Roma.

(Super Eagles)Nigeria na za Tunisia kucheza tena Kombe la dunia.tunisia inaania kucheza kwa mara ya 4 na nusa itie tiketi yake mfukoni,llakini ,bao la dakika za mwisho la nigeria, liliwatilia kitumbua chao mchanga.Hata Algeria, yatazamiwa kurejea Kombe la dunia bada ya kitambo cha miaka 23:

Super eagles-Nigeria, walihitaji bao la firimbi ya mwisho alilotia Obinna kuinyamazisha Msumbiji mjini Abuja,kubakisha matumaini ya kutamba Afrika kusini.Tunisia ililifumania dakika ya kwanza tu lango la harambee Stars-kenya, kuongoza kundi hili kwa pointi 2 ukisalia mchezo mmoja.

Kabla changamoto ya mwisho mwezi ujao, Tunisia itajaribu kutwaa tiketi yao ya kombe la dunia mjini Maputo,wakati Nigeria, lazima ishinde Nairobi,nyumbani mwa Harambee Stars nakutumai Tunisia , inateleza huko Msumbiji.

Jumamosi iliopita,Tembo wa Corte d'Iviore, walikuwa timu ya 3 ya Afrika , kujulikana kuwa itacheza Kombe la dunia baada ya Ghana na wenyeji Bafana Bafana.Tembo wa Ivory Coast, walitosheka na suluhu ya bao 1:1 na Malawi,mjini Blantyre.Simba wa nyika -Kameroun nao, wamepiga hatua kukaribia kujiunga na majirani zao hao wa

Afrika Magharibi- walipo ikandika Togo mabao 3-0.Ushindi wa Kamerun, umewapatia pointi 10 kutoka kundi A,pointi 1 zaidi kuliko Gabon,iliopo nafasi ya pili.

Timu 5 za kileleni mwa kila kundi,zawakilisha Afrika katika Kombe la dunia wakati 3 za usoni kabisa kutoka kila kundi , zitakwenda Angola,Januari mwakani kwa Kombe la Afrika la mataifa.

Mwandishi: Ramadhan Ali

Uhariri: Othman Miraji