Chama tawala cha ANC kinaongoza kwa kura | Matukio ya Afrika | DW | 09.05.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Chama tawala cha ANC kinaongoza kwa kura

Chama tawala nchini Afrika Kusini African National Congress ANC kimeshinda kwa zaidi ya asilimi sitini katika uchaguzi wa bunge na kuendeleza uongozi wa chama hicho .

Uchaguzi wa Afrika Kusini

Uchaguzi wa Afrika Kusini

Chama hicho ambacho kimekuwepo madarakani kwa miaka ishirini sasa tangu kukamilika enzi za ubaguzi wa rangi nchini humo kinamhakikishia Rais Jacob Zuma muhula wa pili madarakani licha ya kuzongwa na kashfa mbali mbali. Caro Robi amezungumza na mwandishi habari Isaac Khomo aliye mjini Johannesburg na kwanza alimuuliza ushindi huu wa ANC una maanisha nini? Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi:Caro Robi

Mhariri: Saumu Yusuf

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

IJUE DW

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com