CAMP PENDELTON ,Carlifonia : Wanamaji 8 washtakiwa | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

CAMP PENDELTON ,Carlifonia : Wanamaji 8 washtakiwa

Waendesha mashtaka kutoka jeshi la Marekani wamewafumgulia mashtaka wanamaji wanane kwa mauaji ya raia 24 wa Iraq wasiokuwa na silaha katika mji wa Haditha nchini Iraq.

Wanajeshi wanne kati yao watakabiliwa na mashtaka ya mauaji wakati wengine wanne itabidi wajieleze kutokana na mashtaka ya kushindwa kuchunguza na kurepoti tukio hilo.Mmojawapo ya wanamaji hao wa cheo cha Sajini Frank Wuterich amefunguliwa mashtaka 13 ya mauaji.Jeshi la Marekani halikusema iwapo mauaji hayo yalikuwa yamepangwa kabla.

Wanajeshi hao wanakabiliwa na adhabu ya juu kabisa ya kifungo cha maisha gerezani.

Mauaji hayo ya Haditha yametokea mwezi wa Novemba mwaka 2005 ikiwa ni kisasi kutokana na kifo cha mwanamaji mwenzao katika mripuko wa bomu lililotegwa barabarani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com