1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameroon yatuma majeshi katika miji mikuu

Caro Robi
22 Oktoba 2018

Majeshi ya Cameroon yametumwa katika miji mikuu huku mikutano ya hadhara ikipigwa marufuku wakati matokeo rasmi ya uchaguzi yakisubiriwa kutangazwa.

https://p.dw.com/p/36w7b
Nordkamerun Grenzregion zu Nigeria Soldaten Anti Terror
Picha: AFP/Getty Images

Majeshi ya Cameroon yametumwa katika miji yote mikubwa nchini humo na mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani imepigwa marufuku kuelekea kutangazwa kwa matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais, ambao unabashiriwa kumpa ushindi Rais Paul Biya ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1982.

Majeshi yameonekana katika makazi ya wagombea urais wa upinzani Maurice Kamto na Cabral Libii ambao wamehamiza Wacameroon kutetea haki zao iwapo watahisi walidanganywa katika uchaguzi wa Oktoba saba.

Waziri Paul Atanga Nji amesmea wanajeshi hawajatumwa mitaani kuwatisha watu bali kuwalinda dhidi ya wanasiasa wanaowachochea vijana kuandamana kupinga asasi za serikali.

Biya mwenye umri wa miaka 85 anayetafuta muhula wa saba madarakani anatarajiwa kushinda kwa urahisi baada ya mahakama ya kikatiba aliyoiteua kupinga kesi zote zilizowasilishwa mahakamani kupinga uchaguzi.