Bush kurushiwa viatu Irak | Magazetini | DW | 16.12.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Bush kurushiwa viatu Irak

kurushiwa viatu rais Bush huko Irak na mjadala iwapo NPD kipigwe marufuku Ujerumani ,ni mada kuu:

G.Bush nchini Irak.

G.Bush nchini Irak.

Uchambuzi wa wahariri wa magazeti ya Ujerumani leo umezungumzia mada mbali mbali kuanzia hatua za kuufufua uchumi,hukumu kwa kampuni la Siemens kwa kutoa rushua hadi kuagwa rais George Bush wa Marekani badala ya kupigiwa m akofi anarupigwa viatu.Mada kuu kabisa iliochambuliwa na wahariri lakini ilikua :je, chama cha wafuasi wenye siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ujerumani (NPD) kipigwe marufuku au la.

Kuhusu kisa cha Rais Bush kuagwa nchini Iraq kwa kurushiwa viatu, gazeti la Mitteldeutsche Zeitung laandika :

"Kururushiwa viatu badala ya kupigiwa makofi ; kutoa hotuba ndani ya ngome iliolindwa kwa viguzo vya seruji,ziara ya kuaga ya George Bush nchini Irak na Afghanistan ,isingeweza kuwa mbaya zaidi.

Bush ameweza kujionea mwenyewe kwa mara nyengine tena na pia kwa mara yake ya mwisho, matunda gani sera za nje za Marekani zimevuna katika nchi zote mbili za msukosuko: yaani,hakuna zilichovuna.

Bila shaka,kujiingiza kwa nguvu kijeshi tangu Irak hata afghanistan kulifaulu kuteketeza tawala za kidikteta,lakini bado sera za Marekani zimeshindwa kujua nini cha kutenda baadae.Hakuna rais wa Marekani alieshindwa kujiuliza: kinafuata nini baada ya uvamizi.

Rais mpya anaefuata Barack Obama ana njia ndefu kwenda kuijenga upya nyumba ilioporomoka uopande huo wa sera za nje....."

Likituchukua katika mada iliochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani- iwapo chama cha NPD cha wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia kipigwe marufuku au la kufuatia kupigwa kisu Polisi huko Pasau, gazeti la Westdeutsche Zeitung laandika:

"Mkasa wa Passau ni ishara ya kuzingatiwa sana kuwa upande wa mrengo wa kulia kabisa wa siasa kali ndani ya jamii yetu kumeibuka kikundi cha walalahoi nje ya jamii kuu ambacho hatukukitia sana maanani.Sasa wanasiasa wanapaswa kukabiliana nacho ,lakini kwa uwazi na kwa hadhari.Baada ya mkabala huo mwishoe itaomnekana kinabidi kupigwa marufuku,wademokrasi wote wataridhia hatua hiyo.Na hata Mahakimu wa Mahkama kuu ya katiba huko Karlsruhe."

Ama gazeti la Kolnischer Rundschau linahisi kiwango kipya kimefikiwa na wafuasi wenye siasa kali katika kumhujumu mkuu wa polisi wa Passau, Bw.Alois Manniche.

Gazeti laongeza:

".....Hiyo si hujuma dhidi ya mtu binafsi tu,bali ni hujuma iliolengwa pia dhidi ya dola analoliwakilisha.Kwahivyo, serikali nayo inabidi kutoa nayo jibu barabara ili kuilinda jamii hii.Serikali ina jukumu hilo kwa mkuu wa polisi huyo wa Passau ambae amekuwa akiulinda mji huo kwa miaka kadhaa na siasa kali...."

Gazeti la Thuringer Allgemeine laandika :

"Je, ni taabu kukipiga marufuku kikosi hiki cha kinazi-mamboleo ? Yadhirika ni hivyo. Chama cha NPD ni wazi kinapinga misingi ya kanuni za katiba,lakini kinaangaliwa kana kwamba kinaendesha shughuli zake kwa muujibu wa katiba ya nchi hii na hakiguswi.

Baada ya kuhujumiwa kikatili kwa mkuu wa polisi wa Passau mjadala motomoto umeibuka sasa kuwa chama hicho kipigwe marufuku...."

Gazeti la Nuremberg Nachrichten limegundua:

"Hasa katika mkoa wa bavaria kwa muuijibu ulivyoonesha uchunguzi wa hivi punde wa kutia wasi wasi, wafuasi wenye siasa kali za kinazi-mambo-leo wana nguvu zaidi kuliko katika mikoa mengine ya Ujerumani:Chuku dhidi ya wakaazi wa kigeni,hisia za kizalendo na zinazowabughudhi wayahudi zikitia fora huko mara kwa mara.Kuwaelimisha na kuwapasha habari ndio njia bora ya kukabiliana nao...."