Burundi: Uchaguzi si wa huru na haki | Matukio ya Afrika | DW | 03.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Burundi: Uchaguzi si wa huru na haki

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa wamesema uchaguzi wa bunge na madiwani uliofanyika siku ya Jumatatu nchini Burundi, haukuwa huru na wa haki.

Parlamentswahlen in Burundi Wahllokal Wahlhelfer Wahlbeteiligung

Uchaguzi wa bunge na madiwani nchini Burundi

Uchaguzi huo uliogubikwa na vurugu na kususiwa na baadhi ya vyama vya upinzani ulifanyika licha ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuitolea mwito serikali ya Burundi kuahirisha uchaguzi huo kufuatia hali mbaya ya kiusalama. Hata hivyo hadi leo raia wa nchi hiyo wanaendelea kusubiria kwa hamu kubwa matokeo hayo yaliokuwa yatolewe rasmi hapo jana. Kwa mengi zaidi juu ya hilo, Amina Abubakar amezungumza na mwandishi wetu Amida Issa aliyeko mjini Bujumbura .

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri:Yusuf Saumu

Sauti na Vidio Kuhusu Mada