1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiKenya

Bunge la Kenya lapitisha muswada tata wa fedha

Bruce Amani
22 Juni 2023

Bunge la Kenya jana usiku limepiga kura ya kuidhinisha muswada tata wa fedha, utakaoongeza kodi ya mafuta mara mbili na kuanzisha kodi mpya ya nyumba, katika hatua inayoashiria ushindi kwa Rais William Ruto.

https://p.dw.com/p/4SvBB
Kenia Haushalt 2023 | Finanzminister Njuguna Ndung'u
Picha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Bunge la Kenya jana usiku limepiga kura ya kuidhinisha muswada tata wa fedha, utakaoongeza kodi ya mafuta mara mbili na kuanzisha kodi mpya ya nyumba, katika hatua inayoashiria ushindi kwa Rais William Ruto. Muswada huo sasa utapelekwa kwa rais kwa ajili ya kusainiwa.

Kwenye mjadala huo uliokwenda hadi usiku wa manane, wabunge kutoka upande wa Ruto walifanikiwa kuyashinda majaribio ya upinzani ya kuzuia ongezeko la kodi ya mafuta pamoja na kodi mpya ya nyumba ya asilimia 1.5 itakayokatwa kwa wafanyakazi.

Upinzani ulitishia kuitisha maandamano mapya iwapo Ruto atasaini muswada huo na kuwa sheria, ingawa serikali ya Ruto inasisitiza juu ya umuhimu wa kupandisha viwango vya kodi ili kuweza kukabiliana na changamoto za kifedha zilizoongezeka kutokana na ulipaji wa deni na makusanyo duni ya ushuru.

RTE