Bundesliga. | Michezo | DW | 01.11.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bundesliga.

Borussia Dortmund waongoza Bundesliga.

default

Mario Goetze wa timu ya Dortmund akifunga bao.

Borussia Dortmund ndiyo wanayoishikilia bendera ya ligi hii baada ya kuwanyamazisha Mainz kwa mabao 2-0 kupitia chipukizi wake Mario Goetze na mfungaji Lucas Barrios.

Mafarasi weusi Mainz, walishindwa kufunga Penalti baada ya kapteni wa Dortmund Roman Weidenfeller alipouzuiwa mkwaju huo na kwa wakati wote Mainz walishindwa kuwahimili vijana wa Jurgen Klopp katika kindumbwe ndumbwe hicho kilichogaragazwa ugani Bruchwegstadion.

Mkufunzi Klopp amesema ushindi huo ni kutokana na ujuzi wao dimbani wa kusakata soka na haikuwa kazi rahisi .

Deutschland Kombo Fußball Trainer Jürgen Klopp und Thomas Tuchel

Kocha Jürgen Klopp wa Borussia Dortmund na mwenziwe wa Mainz Thomas Tuchel .

Ushindi huo umeipa Dortmund uongozi wa pointi moja dhidi Mainz walioshuka hadi nafasi ya pili katika ligi hiyo baada ya mechi zake kumi.

Wageni Dortmund walitangulia kukibusu kimia cha Mainz kunako dakika 26 wakati chipukizi Goetze mwenye umri wa miaka 18 alipomshambulia mlinzi wa Mainz Niko Bungert na kufunga goli hilo la kwanza.

Mparaguay Lucas Barrios alisukuma tobwe la pili kunako dakika 67 ya mchuano huo na kuipa timu yake ya Dortmund ushindi.

Baadaye timu ya Hoffeinheim ilichukuwa nafasi ya tatu katika ligi hiyo ya Bundesliga kwa kichapo ilioipa Hannover 96 ya mabao 4 kwa mshangao.

Mchezaji wake wa kiungo cha kati Gylfi Sigurdsson alichangia mawili kati ya mabao hayo manne.

Na mambo yalionekana kutokuwa mazuri kwa Werder Bremen na Schalke 04 juzi Katika michuano iliyotazamwa kuwa mazoezi kwa mechi za hapo kesho ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambapo timu zote mbili zilifungwa nyumbani.

Werder Bremen waliofungwa nyumbani na Nuremberg mabao 3-2, wanawakaribisha mabingwa wa ligi ya uholanzi FC Twente katika kundi A . Huku nao Schalke baada yakufungwa bao 1-0 na Leverkusen, wanasafiri hadi Tel aviv watakakopambana na timu ya Hapoel katika kundi B.

Kwa sasa Leverkusen ipo katika nafasi ya nne katika ligi ya Bundesliga kutokana na ushindi huo, huku timu ya Eintracht Franfurt wakiwa watano baada ya ushindi wao wa mabao 3-1 dhidi St.Pauli.

Mabingwa Bayern Munich wanaonekana kujivuta vuta katika ligi hiyo, baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi Freiburg mwishoni mwa juma.

Mwandishi Maryam Abdalla/AFPE

Mhariri:Othman Miraji

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com