Bundesliga. | Michezo | DW | 01.10.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bundesliga.

Mainz inapambana na Hoffeinham huku Bayern Munich dhidi Dortmund.

FSV Mainz 05

FSV Mainz 05

Timu inayoendelea kuwaacha wengi kanwa wazi, Mainz, inaelekea kuandika historia mpya katika Bundesliga hapo kesho watakapokabiliana na Hoffeinheim na kudhihirisha kuwa uwanjani, ndiko kwao. Huku Mabingwa Bayern Munich wanatarajia kuondosha tahayuri dhidi Dortmund siku ya Jumapili.

Mpaka sasa ni Kaiserslautern mnamo mwaka 2001/2002 na mabingwa Bayern Munich mnamo mwaka 1995/96 waliowahi kushinda mechi zao zote saba za ufunguzi wa Bundesliga.

Kwa kasi iliyo nayo Mainz, huenda ikawa timu ya tatu kuweka rekodi hiyo, kwa kuongeza ushindi kwenye mechi zake saba muruwa inayojumuisha hii ya leo dhidi Hoffeinheim.

Ni ushindi muruwa, ikizingatiwa jazba waliokuwa nayo dhidi Bayern Munich Jumamosi iliopita kwa kuilaza mabao 2-1.

Umahiri wa usakataji soka wa chipukizi, kiungo cha kati, Lewis Holtby mwenye umri wa miaka 20 na mfungaji Andre Schuerrle walio funga mabao 5 kati yao unaonekana kumsisimua pia kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew.

Hatahivyo mashamsham haya yote, mkufunzi wa timu hiyo ya Mainz, Kocha Thomas Tuchel, ana yaweka kando kwa kusema hana muda wa kuota ndoto, na badala yake ni uwajibikaji uwanjani tu, kujaribu kufanya mabadiliko katika kuorodheshwa kwa timu hiyo katika mashindano hayo ya bundesliga ambayo Mainz tangu mwongo uliopita haijafanikiwa kukwea zaidi ya nafasi ya nne kwenye orodha ya timu hizo za Ujerumani.

1. FSV Mainz 05 gegen 1. FC Koeln

Kocha Thomas Tuchel na mchezaji wake Andreas Ivanschitz.


Timu ya Hoffeinheim ni ya nne kwenye meza hiyo, lakini ina pointi 7 nyuma ya Mainz ilio na pointi 18.

Kwa upande wake bingwa wa ligi hiyo ya Ujerumani, Bayern Munich, wanatarajia kujizatiti kuondosha tahayuri ya Jumamosi iliopita katika uwanja wake wa Allianz, watakapo kabiliana na Dortmund.

Bayern mpaka sasa ni wa tisa katika ligi hiyo wakiwa na pointi 8 katika mechi zake 6, huku Dortmund ikiwa ya pili katika ligi hiyo nao wanapeperusha bendera yao juu zaidi huku kapteni Mark van Bommel, ambaye upande wake ulipata ushinda dhidi Basela katika mashindano ya mabingwa barani Ulaya mapema wiki hii, amesema ni ushindi tu wanaoutafuta watakapo pambana na mabingwa Bayern ili kuepuka kufuatwa unyo unyo na waandishi habari wa Ujerumani.

Na katika mechi nyingine kwenye ligi hii ya Bundesliga,

Weder bremen wana nafasi ya kufufuka kutoka kwa mpigo wa 4- 0 walioupokea kutoka kwa watetezi wa taji la mabingwa barani Ulaya Inter milan watakapo onana na Leverkusen siku ya Jumapili.

Schalke 04 nayo inaonyesha umahiri wake wa usakataji ngozi iliyoambwa na kutengenezwa mpira dhidi Nuremberg.

Stuttgart kwa upande wake inapania kujizatiti kuondoka kwenye nafasi za chini katika ligi hii watakapowakaribisha Eintracht Frankfurt Jumapili.

Mwandishi: Maryam Abdalla/AFPE

Mhariri:Josephat Charo