Bundesliga yarudi uwanjani | Michezo | DW | 14.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bundesliga yarudi uwanjani

Mpambano kati ya Bayern munich na schalke utagubikwa na uhasama wa dimba wa ndugu 2 wa kituruki-Halil na Hamit Alitintop.Pia washambulizi 2:

Bundesliga uwanjani leo

Bundesliga uwanjani leo

Leo Bundesliga-Ligi ya Ujerumani, inarudi uwanjani baada ya likizo ya wiki mbili kuiruhusu timu ya taifa kuania tiketi ya finali za kombe la Ulaya hapo mwakani huko Uswisi.

Ndugu wawili wa kituruki mmoja akiichezea Bayern Munich na mwengine Schalke Hamit na halil Altintop hawatavunja udugu wao leo pale timu zao mbili hasimu zitakapopambana kwa changamoto ya Bundesliga.Hata Premier League-ligi ya Uingereza iko uwanjani leo –mabingwa Manchester wana miadi na Everton.

Ndugu hao 2 akina Halil na Hamit Alitintop wanazungumza kila mara licha ya kuwa mmoja aichezea Munich na mweengine Schalke.Juzi tu walikuwa chumba kimoja mjini Istanbul,kabla Uturuki kuilaza Hungary mabao 3:0 katika kuania tiketi ya Euro 2008-komb e la Ulaya la mataifa.

Bayern Munich inasubiri kupona kwa mshambulizi wao wa Itali,Luca Toni wakati mlinzi wao Philipp Lahm,si fit kabiosa kucheza.Changamoto ya jioni ya leo itawapambanisha pia washambulizi 2 wa timu ya Taifa:Kevin Kuranyi wa schalke na Miroslav Klose wa Munich.

Mabingwa Stuttgart wana miadi nyumbani na Energie Cottbus wakati Bayer Leverkusen inaiklaribisha Bochum.Nuremberg inacheza na Hannover.Arminia Bielefeld inakumbana na Hansa Rostock na Frankfurt inahetimisha duru ya leo kwa mpambano wake na Hamburg.

Kesho jumapili mapambano 2 yatakamilisha duru hii ya Bundesliga:Wolfsburg itacheza na Karsruhe wakati Duisburg iatumana na Hertha Berlin.

Ama katika premier League ,Ligi ya uingereza mabingwa Manchester united wafunga safari kuitembelea Everton kwa nia ya kuwapokonya pointi 3.

Chelsea wanacheza nyumbani na Blackburn Rovers wakati Arsenal inaitembelea Tottenham Hotspur.Kesho jumaöili, Manchester city inacheza na Aston Villa huku Derby County na Newcastle United wakiilaza ngoma uporo hadi jumatatu.

Kombe la dunia la wanawake linaendelea huko China.Australia na kanada zinarudi leo uwanjani kila moja ikipania kunyakua nafasi ya pili kutoka kundi C.Norway imeshaparamia kileleni mwa kundi hilo baada ya kuilaza Kanada 2-1.Australia ilitimua Ghana 4-1.Leo Norway inacheza na Australia wakati Ghana ina miadi na kanada.

Katika kombe la dunia la rugby nchini Ufaransa, Ureno inayoshiriki kwa mara ya kwanza ina miadi leo na New Zealand na ikiwa haitachunga itakiona kilichomtoa kanga manyoya kutoka kwa all-Blacks.Kocha wa New Zealand Graham Henry amefanya mageuzi 11 katika kikosi kilichoizaba Itali mabao 76-14.

Jana mabingwa Uingereza walikuwa uwanjani na Springbox-Afrika Kusini walioanza kwa kishind.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com