Bundesliga yaanza tena leo | Michezo | DW | 01.02.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bundesliga yaanza tena leo

Kombe la Afrika lapumzika leo hadi kesho,lakini Bundesliga imerudi uwanjani kwa kishindo.

default

Jürgen Klinsmann -kocha mpya wa B.Munich Julai mosi.

Wakati Bundesliga-Ligi ya Ujerumani inarudi tena uwanjani leo kwa mpambano mengine baaada ya jana ijumaa viongozi wa Ligi-Bayern Munich na Hansa Rostock kufungua dimba la duru hii ya pili ya msimu, kombe la Afrika la Mataifa linapumzika leo hadi kesho jumapili pale wenyeji Ghana watakapopapurana na mahasimu wao wa jadi-Nigeria. Mpambano wapili kesho utakua kati ya Corte d’Iviore-Ivory Coast na Guinea.

Oumilkheir anatufumnulia kawa la changamoto za kesho za Kombe la Afrika na Bundesliga hii leo:

Kesho wenyeji Ghana wanaanza duru ya pili kwa mpambano wa kukata na shoka na mahasimu wao wa jadi huko Afrika magharibi-Nigeria.Hatima ya kila timu itajulikana baada ya firimbi ya mwisho mjini Accra.

Ghana ikiwa inacheza nyumbani,haingependa kuliaga kombe la Afrika na mapema.Nigeria nayo,kulazwa tu na mahasimu wao wa jadi Ghana ni udhia mkubwa.

Corte d’Iviore-Ivory Coast siku hiyo hiyo ina miadi na Guinea huko Sekondi,na kocha wao -mfaransa Gerard Gili anadai Tembo wamejifunza darasa walilopata kutoka kombe lililopita la dunia hapa ujerumani 2006 katika kiu chao cha kutwaa ubingwa mara hii-ubingwa waliokosea kidogo tu 2006 huko Cairo. Kama wenyeji-Ghana, Ivory Coast haikupoteza pointi-imeshinda mapambano yake yote 3 ya kwanza.Kutoka Kombe lililopita la dunia hapa Ujerumani 2006,tembo-asema kocha wao Gerrad Gili, walijifunza vipi kuhimili vishindo vya mechi ngumu.Ivory Coast,ililazwa na Holland na Argentina kwa mabao 2:1 hata,lakini iliilaza Serbia 3-2.

Mshambulizi wao anaechezea Bundesliga-Boubacar Sanogo anadai „Ivory Coast sasa haimuogopi yeyote tena hata wenyeji Ghana..“

Je, Ivory Coast hawaiogopi pia mabingwa Misri,waliowapokonya kombe 2006 mjini Cairo baada ya changamoto za mikwaju ya penalty?.Misri ina miadi jumatatu na Angola na kocha wao Luis Oliveira Goncalves,baada ya timu yake kutoka sare jana bao 0:0 na Tunesia,adai Angola imethibitisha kwamba majina ya timu hayashindi mechi za dimba.Kibarua cha Angola mjini Kumasi,jumatatu hatahivyo, hakitakua rahisi,kwani mabingwa Misri,hawatotaka kuliachia kombe kubaki Accra na wao kurudi Cairo mikono mitupu.

Misri iliwahi kutamba Afrika magharibi hapo 1998 waliporudi na kombe Cairo kutoka Burkina Faso.

Bundesliga inarudi uwanjani jioni hii baada ya likizo ya X-masi na mwaka mpya: Viongozi wa Ligi-Bayern Munich walifungua duru hii ya pili ya msimu hapo jana kwa changamoto na Hansa Rostock wakati katika Ligi ya daraja ya pili-FC cologne ilikua na miadi nyumbani na St.Pauli.

Changamoto nyengine leo kati ya Energie Cottbus na Bayer Leverkusen wakati Karlsruhe ina miadi na Nuremberg.Duisburg inaumana na Borussia dortmund wakati Armenia Bielefeld inapambana na Wolfsburg.

Kesho jumapili, duru hii ya kwanza ya rauni ya pili ya msimu huu itakamilishwa kwa mapambano 2: Schalke 04 ina miadi na Stuttgart wakati Werder Bremen inaikaribisha nyumbani Bochum.Schalke itabidi kuchunga kwani jogoo la stuttgart lililochaguliwa „mwanasoka bora wa mwaka „ wa Ujerumasni mario Gomez limerudi uwanjani wiki hii kwa vishindo.Ametia mabao 3 pekee kuikatia Stuttgart tiketi ya robo-finali ya kombe la Ujerumani tena ilikua katika lango la Werder Bremen.

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com