Bundesliga kuchelewesha ′spray′ inayofutika haraka? | Michezo | DW | 27.09.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bundesliga kuchelewesha 'spray' inayofutika haraka?

Matumizi ya spray inayofutika haraka wakati wa kupigwa mipira ya freekick, katika Bundesliga huenda yakacheleweshwa kwa sababu bidhaa hiyo kutoka Argentina inayostahili kutumiwa, haijaidhinishwa

Kampuni inayokagua ubora wa bidhaa ya Ujerumani – TUEV imesema bidhaa huyo kutoka Amerika ya Kusini ina vitu ambavyo haviruhusiwi katika bidhaa za aina hiyo nchini Ujerumani na kwamba maandishi yaliyoko kwenye bidhaa hiyo hayajakamilika na hayako katika lugha ya Kijerumani.

Msemaji wa kampuni hiyo ya TUEV Ralf Dieckmann amesema bidhaa hiyo katika mfumo wake sa sasa haiwezi kutumika nchini Ujerumani na katika Umoja wa Ulaya. Shirika la Kandanda la Ujerumani DFB limesema halifahamu chohcote kuhusu uamuzi wa TUEV lakini limezungumza na kampuni nyingine zinazotengeneza bidhaa hizo ili kuepuka gharama kubwa ya uagizaji kutoka Argentina.

DFB inapanga kuzindua matumizi ya spray inayofutika kwa haraka, ambayo inatumika wakati wa mipira ya free kick, kuanzia Septemba 18/19 kuendelea mbele baada ya kufaulu katika Kombe la Dunia. Tayari inatumika katika ligi kadhaa za Ulaya ikiwa ni pamoja na England na Champions League.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/DPA
Mhariri: Mohammed KHELEF