Bundesliga kuanza leo jioni | Michezo | DW | 20.08.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bundesliga kuanza leo jioni

Mabingwa watetezi wa ligi ya Bundesliga- ligi ya Ujerumani Bayern Munich wanaanza kulitetea taji leo jioni hii, nyumbani katika uwanja wa Allianz Arena dhidi ya Wolsburg.

Ligi ya Bundesliga kuanza jioni hii.

Ligi ya Bundesliga kuanza jioni hii.

Bayern ambao msimu uliopita walitwaa mataji mawili, wanawania safari hii kutoroka na taji la 23 la mabingwa wa Ujerumani. Makamu wa mabingwa Schalke wanaingia uwanjani kesho huku kocha wao Felix Magath akitishia kujiuzulu kutoka timu hiyo kuna ni?

Uwanjani Allianz Arena mabingwa watetezi Bayern Munich wanaanza kulitetea taji lao, jioni hii dhidi ya Wolsburg. Bayern hata hivyo wanaumishwa kichwa kwa kuwa watawakosa wachezaji stadi Arjen Robben na Ivica Olic . Robben anauguza jeraha la mguu alilopata wakati wa fainali ya kombe la dunia huko Afrika Kusini, ilhali Mcroatia Olic anauguza jeraha la goti.

Flash-Galerie Deutschland Wochenrückblick 2010 KW 33 Bundesliga beginnt

Bayern Munich ndio mabingwa watetezi

Nahodha Marc Van Bommel pia ana harakati za kuwa fit, na iwapo atakosekana mzigo wa kusimamia ulingo wa kiungo cha kati cha bayern utamuangukia Daniel Pranjic. Mechi Alllianz Arena pia itakuwa ya kwanza ya kocha mpya wa Wolsburg Muingereza Steve McClaren anayekuwa kocha wa kwanza Muingereza katika Bundesliga.

McClaren anasemémaka yuko mbioni kumsaka mshambulizi wa Liverpool Ryan Babel na Mbrazil Diego kutoka Juventus

Schalke ambao waliwatoa kijasho Bayern msimu uliopita na ambao ni makamu wa mabingwa wataingia uwanjani kesho dhidi ya Hamburg......Lakini uwanjani haitokuwa kusakata kabumbu tu...kuna wasiwasi Schalke baada ya Kocha Felix Magat kutishia kwamba kwamba huenda akajiuzulu kutokana na kashfa anazopata kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo. Lakini Magat anaelekeza fikra zake zote kwa mechi dhidi ya Hamburg, Magat anasema

Felix Magath Schalke Bundesliga

Felix Magath kocha wa Schalke atishia kujiuzu.

Mechi kati ya Schalke na Hamburg itawaleta pamoja uwanjani wachezaji wawili wa zamani wa Real Madrid- Raul ambaye atakuwa amevalia jezi ya Schalke na Ruud Van Nistelrooy akiongoza mashambulizi ya Hamburg.

Werder Bremen ambao kati kati ya wiki walisahau majonzi ya kumuuza mchezaji wao nyota Mesut Ozil kwa Real Madrid walipowazaba Sampdoria mabao 3-1 katika mechi ya kufuzu kwa dimba la Champions League- pia leo walikuwa wageni wa Hoffenheim.

Mechi zingine za kesho,Borussia M'gladbach watawaalika Nuremberg, huku Cologne ikiikaribisha Kaiserslauetern. Hannover itacheza na Frankfurt Eintracht

Jumapili Bayer leverkusen ambao wanamkaribisha nyota wao wa zamani Michel Ballack watakuwa nyumbani kwa Borrussia Dortmund ilhali Stutgart itakuwa na miadi na Mainz.

Flash-Galerie Bundesliga 9. Spieltag FSV Mainz 05 gegen SV Werder Bremen

Timu ya Werder Bremen.

Na kufuatia kampeini kabambe ya timu ya Ujerumani katika michuano ya kombe la dunia huko Afrika Kusini- matunda sasa ni kwamba mauzo ya tiketi za mechi za Bundesliga yameomgezeka mno na kuwa ya juu sana katiika historia ya Bundesliga.

Timu zote 18 za Bundelisga zimeripoti kuwa zinauza kwa wingi tiketi za mechi zake- kwa ujumla sasa wameuza tiketi laki nne na elfu sitini ukilinganisha na laki nne na elfu 30 msimu uliopita.

Timu ya Borussia Dortmund ndio inaongoza kwa kuuza tiketi nyingi msimu huu ambao ligi imeanza jana rasmi. Dortmund wanaripoti wameuaza tiketi elfu 51 na mia mbili, ukilinganisha na msimu uliopita walipouta tiketi elfu 50. Dortmund walimaliza katika nafasi ya tano msimu uliopita Schalke imechukua nafasi ya pili kwa mauzo ya juu ya tiketi, ilhali mabingwa Bayern Munich waliacha kuuza tiketi za mechi katika uwanja wa Allianz Arena walipouza tiketi elfu 37, na mia sita.

......................................................... Mwandishi: Munira Muhammad/afpe, rtre Mhariri: Josephat Charo