Bundesliga Jumamosi | Michezo | DW | 07.11.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bundesliga Jumamosi

Viongozi wa Ligi Dortmund leo wako unwanjani kupambana na Hanover.

default

Marcel Schmelzer wa Dortmund.

Katika mechi zilizochezwa jumamosi katika Bundesliga Ligi ya hapa Ujerumani, Mainz wamesalia katika nafasi ya pili baada ya kushindwa kwa bao 1-0 na Freiburg. Kwengineko mlinzi wa Bayern Munich Philip Lahm aliikoa timu hiyo kwa bao lake katika dakika ya 84, na kusawazisha mabao 3-3 dhidi ya Borussia Monchengladbach.

Fußball Bundesliga SC Freiburg gegen FSV Mainz 05 Flash-Galerie

Mchezaji wa Mainz Eugen Polanski (kulia) na Freiburgs Anton Putsila wa Freiburg.

Katika mechi nyingine Frankfurt iliicharaza Wolfsburg 3-1. Cologne nayo haikuwa na bahati mbele ya Nürnberg walipofungwa mabao 3-1. Hoffenheim nao walionyeshwa kidumbwedumbwe na Hamburg kwa kichapo cha mabao 2-1.

Viongozi wa Ligi Borussia Dortmund wako uwanjani leo wakiwa na matumaini ya kuendelea kusalia kileleni wiki ijaayo. Wapinzani wao ni Hanover.

Fußball Spanien Liga Real Madrid Racing Santander

Christiano Ronaldo wa Real Madrid.

Kwingineko Bayer Leverkusen watawaalika Kaiserslautern ilhali VFB Stutgart itamenyana na Werder Bremen.

Katika Premia Ligi, viongozi wa ligi Chelsea leo wana miadi na vijana wa Roy Hodgson, Liverpool huko Anfield. Arsenal watakuwa nyumbani Emirates dhidi ya Newcastle.

Katika La Liga ligi ya Spain - viongozi wa ligi Real Madrid wana kibarua dhidi ya majirani zao Atletico Madrid katika mechi maarufu kama " Madrid derby".

Mabingwa Barcelona nao watawakaribisha Getafe.