Bremen yaituliza kasi ya Leverkusen kileleni | Michezo | DW | 13.09.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Bremen yaituliza kasi ya Leverkusen kileleni

Viongozi wa mapema wa ligi Bayer Leverkusen waliangusha points za kwanza msimu huu baada ya kutoka sare ya kufungana magoli matatu kwa matatu na Werder Bremen hapo jana

Mechi hiyo ya kukata na shoka ingeweza kukamilika katika kipindi cha kwanza pekee. Wenyeji Leverkusen waliongoza kutoka mwanzo kutokana na goli la Tin Tedvaj na wakakosa kutikisa wavu baada ya mpira kugonga mwamba mara tatu.

Bremen walibadilisha mambo kupitia wachezaji Fin Bartels na Franco Di Santo kabla ya Leverkusen kurudi nyuma kutoka usingizini kwa kufunga magoli mawili na kufanya mambo kuwa 3-2 kupitia Hakan Calanoglu na Son Heung Min.

Bremen hawakusinzia hata kidogo na nahodha wao Sebastian Proedl akafunga na kufanya mambo kuwa 3-3 zikiwa zimesalia dakika tano mchuano kukamilika. Mechi nyingine zinachezwa kwa sasa.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman