BRAZAVILLE: Kura zimeanza kuhesabiwa
25 Juni 2007Matangazo
Kura zimeanza kuhesabiwa baaada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge nchini Jamuhuri ya Kongo Brazaville, lakini habari zinasema kuwa idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo na tume ya uchaguzi imesema kuwa makosa yamefanyika.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kufahamika baada ya wiki moja.
Vyama 40 vya kisiasa vimesusia uchaguzi huo kwa madai kwamba una lengo la kuimarisha utawala wa rais Denis Sassou-Nguesso ambae ameishakaa madarakani kwa muda wa miaka 23.