1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BP kupata mkurugenzi mpya

28 Julai 2010

Kampuni ya mafuta ya Uingereza,BP imetangaza kuwa mkurugenzi mkuu anayeondoka madarakani Tony Hayward,atajiuzulu rasmi ifikapo Oktoba mosi

https://p.dw.com/p/OWBb
Nembo ya BPPicha: BP

Wadhifa huo utamuendea Bob Dudley,ambaye ni Mmarekani.Kampuni hiyo kubwa  ya mafuta  inajitahidi kulisafisha jina lake huko Marekani kufuatia ajali ya  kisima kuvuja mafuta yaliyotanda kwenye eneo la Ghuba ya Mexico.Dudley amekuwa akisimamia  operesheni za kulisafisha eneo hilo na ameahidi kufanya kila linalohitajika kulisafisha  pia jina la kampuni  hiyo.

BP / Ölpest / Golf / Mexiko / USA
Kizibo kwenye kisima cha mafuta kilichokuwa kikivuja katika Ghuba ya MexicoPicha: AP

Bob Dudley amekiri kuwa kampuni ya mafuta ya BP  imejifunza mengi kwasababu  ya mkasa huo  na kutokana  na hilo wataiimarisha taasisi hiyo.Ajali hiyo imesababisha hasara ya kiasi  cha  dola  bilioni 17 katika kipindi cha robo ya  pili ya mwaka.Hasara  ya namna hiyo haijawahi kushuhudiwa kwenye robo ya pili  ya mwaka katika historia ya biashara ya Uingereza.Hayward  ataendelea kuwa msimamizi wa viwanda vya BP vilivyoko Urusi.                

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa,wanaeleza kuwa Bp pia inakabiliwa na shutuma nzito za kulihusisha kampuni hilo kushinikiza kuachiwa mtuhumiwa wa uripuaji ndege ya Lockerbie raia wa Libya, Abdelbaset Ali Mohment al-Megrahi ili kuweza kupata kandarasi ya kuchimba mafuta nchini Libya,kufuatia kurega rega kwa uhusiano baina ya Marekani na Uingereza. Baraza la seneti la masuala ya nje la Marekani,linatarajiwa kukutana Alhamisi wiki hii,juu ya uwezekano wa kuhusishwa kwa kampuni ya Bp,na kuachiwa kwa Al Megrahi,raia pekee aliyehukumiwa kufuatia tukio la kigaidi la mwaka 1988,lililosababisha vifo vya raia 270,huko Scotland,na kuamua kumuachia huru kufuatia kuugua ugonjwa wa kansa. Lakini Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza,William Hague amepeleka maelezo yake kwa baraza la seneti la Marekani,na kueleza kuwa baraza hilo linapaswa kuchukuwa jukumu lake kwa kukanusha tuhuma zinazohusisha kuachiwa kwa Megrahi,kumechangiwa na ushawishi wa kampuni ya Bp. Hata hivyo,Hague ameeleza kuwepo mawasiliano yasiyo na shaka baina ya viongozi wa ngazi za juu wa Bp na serikali ya Uingereza,juu ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa,baina ya Libya na Uingereza na kusainiwa mwaka 2008,lakini amesisitiza kuwa kuachiwa kwa Megrahi,hakuhusiani na mawasiliano hayo.