Bora subira kuliko kishindo | Matukio ya Kisiasa | DW | 22.07.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Bora subira kuliko kishindo

Kishindo kilichowakaba viongozi wa Umoja wa sarafu wakati wa mkutano wao wa kusaka namna ya kuiokoa Ugiriki isizame katika bahari ya madeni

default

Ugiriki yafarajiwa

Si hisani kubwa hivyo ikilinganishwa na jinsi wengi walivyokuwa wakitarajia:yaani wote wanawajibika kwa pamoja katika kuihifadhi kanda ya Euro dhidi ya walanguzi,mfano kwa mataifa yanayojimudu na yale yanayodaiwa kukopa kwa kiwango sawa cha riba na kudhaminiwa na fuko maalum la kuhifadhi sarafu ya Euro.Hivyo ndivyo baadhi walivyofikiria.

Lakini pia sauti zinaongezeka,na sio tu nchini Ujerumani za wale wanaotaka pawepo kikomo.Yote haya yataishia wapi?Ndo kusema hivi karibuni patahitajika pia fungu la pili la msaada kwa Ireland,Ureno na fungu la msaada kwa Hispania na Italy?Lini watu watapumua?Na zaidi kuliko yote itawezekanaje kuwa na bajeti hafifu,ikiwa kila wakati kunazuka jengine?Ottmar Issing,mkuu wa zamani wa benki kuu ya Ulaya anahisi kama masharti ya mkopo yangebadilishwa basi Ugiriki ingelazimika kutoka kwenye umoja wa sarafu. Matokeo yake yamepindukia-lakini shaka shaka zilizoko zinaonyesha ni za kueleweka.

Treffen Merkel Sarkozy Berlin Euro-Sondergipfel

Kansela Angela Merkel na rais wa Ufaransa Sarkozy

Madai na matarajio ya siku za nyuma yalikuwa yakilenga kati ya ncha hizo mbili .Lakini kama kansela Angela Merkel alivyokwishasema,pumzi hasa watu bado hawajazishusha.Ingawa kuhusishwa wafadhili wa kibinafsi ni hatua mpya,lakini uamuzi wa kuzuwia sehemu ya madeni umewekewa kikomo cha siku kadhaa tuu na kudhaminiwa na fuko la kuiokoa sarafu ya Euro.

Ugiriki ,kwa kupatiwa mpango wa kuiokoa "Marshall Plan",itaweza upya sasa kuvuta pumzi.Na sio peke Ugiriki,lakini na zile nchi mbili nyengine zinazohitaji kusaidiwa yaani Ureno na Ireland zinastahiki kupatiwa mkopo kwa riba nafuu ili uchumi wao uweze kunusurika.

Ikilinganishwa na hali namna ilivyokuwa hadi hivi karibuni ,mtu anaweza kusema yaliyofikiwa si haba.

Lakini suala ni inatosha?Haimaanishi kituo kuona eti masoko ya hisa yameupokea vyema uamuzi uliofikiwa mjini Brussels.Kwasababu kila baada ya mkutano wa kilele watu walikuwa wakiamini hatimae watu wangepumua.Miezi michache baadae,mkutano mwengine wa kilele unafuatia ili kutoa ishara bayana kwa masoko ya hisa.

Euro Eurokrise Europäische Länder in der Schuldenkrise Flash-Galerie

Kitambulisho cha mgogoro wa sarafu ya Euro

Hata hivyo uamuzi uliofikiwa unastahiki kuzingatiwa.Hatua za kutisha wengi waliokuwa wakizitaka zingekuwa na madhara ya kutisha pia pindi mambo yangekwenda kombo.Kwa hivyo bora mikutano ya kilele hata kama kuna watatu utakaoitishwa.

Mwandishi:Hasselbach Christoph/Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Miraji Othman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com