Bondia Mayweather kurejea ulingoni? | Michezo | DW | 10.05.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Bondia Mayweather kurejea ulingoni?

Floyd Mayweather ameendelea kutia mafuta katika moto kwa uwezekano wa kurejea katika ulingo baada ya bingwa huyo mstaafu kudokeza kuwapo na uwezekano wa kupambana dhidi ya Conor McGregor wa Ireland

Kukiwa na ripoti hivi karibuni zinazodai kwamba wapiganaji hao wawili wanaogonga vichwa vya habari wanajadili pambano hilo, Mayweather ameuchochea uvumi huo pembezoni mwa pambano la Canelo Alvarez na Amir Khan mjini Las Vegas mwishoni mwa juma.

Mpiganaji huyo raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 39 alistaafu Septemba mwaka jana baada ya kupata ushindi mara 49 katika kipindi cha miaka 19 ya kupigana ngumu ambapo alipata mataji ya dunia katika viwango vitano vya uzito na kujipatia kiasi cha dola milioni 800.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri: Iddi sessanga

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com