Bomu laua watu 50. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Bomu laua watu 50.

Islamabad.

Polisi wa Pakistan wamewakamata watuhumiwa kadha kwa kuhusika na shambulizi la bomu la kujitoa muhanga ambalo limesababisha vifo vya watu wapatao 50 na kuwajeruhi zaidi ya 100 wengine kaskazini magharibi ya nchi hiyo.

Mlipuko huo ulitokea katika msikiti ambao ulikuwa umejaa watu karibu na mji wa Peshawar wakati wa swala ya Ijumaa.

Inafikiriwa kuwa mlipuko huo ulikuwa ni jaribio la kumuua waziri wa mambo ya ndani anayeondoka madarakani Aftab Sherpao, ambaye amenusurika. Hilo ni shambulio la pili la kujitoa muhanga katika muda wa miezi minane iliyopita likimlenga Sherpao, ambaye ni mshirika wa karibu wa rais Pervez Musharraf na amekuwa mtu muhimu katika mapambano ya Pakistan dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com