Boko Haram yauwa wanajeshi watatu wa Nigeria | Matukio ya Afrika | DW | 29.11.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Boko Haram yauwa wanajeshi watatu wa Nigeria

Wapiganaji  wa kundi  la  Boko  Haram  wamewauwa wanajeshi  watatu  katika  shambulio  dhidi  ya  kituo  cha jeshi  kaskazini  mashariki  mwa  jimbo  la  Nigeria.

Wapiganaji  wa kundi  la  Boko  Haram  wamewauwa wanajeshi  watatu  katika  shambulio  dhidi  ya  kituo  cha jeshi  kaskazini  mashariki  mwa  jimbo  la  Nigeria  la Borno  karibu  na  Ziwa  Chad, duru  za  kijeshi  na  raia zimesema.

Wapiganaji  wa  kundi  lijiitalo Dola  la  Kiislamu  la  Afrika Magharibi  wakiwa  na  magari  kadhaa  walishambulia kituo  hicho  cha  jeshi  katika  kijiji  cha  Cross-Kauwa  siku ya  Jumanne na  kupambana  na  majeshi  katika mapambano  ya  saa  nzima.

Afisa  mmoja  wa  jeshi  amesema  wanajeshi  walipambana na  wapiganaji  hao  lakini  walielemewa  na  walilazimika kujiondoa  kutoka  katika  kituo  hicho. 

Tangu  Julai  shirika  la  AFP limeorodhesha  mashambulizi 17  katika  vituo  vya  kijeshi,  ambapo mengi  yao yamedaiwa kufanywa na kundi  hilo lijiitalo Dola  la Kiislamu  la  Afrika  Magharibi.