1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken aomba mataifa ya Kiarabu kuishinikiza Hamas

10 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewarai viongozi wa Mashariki ya Kati kuishinikiza Hamas kukubaliana na pendekezo la Marekani la mapatano kati yake na Israel.

https://p.dw.com/p/4gsdC
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameendelea kutoa wito kwa Hamas kukubali pendekezo la Rais Joe Biden la kusitisha mapiganoPicha: Vadim Ghirda/AP/dpa/picture alliance

Akizungumza baada ya kukutana na Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri huko Cairo, Blinken amesema Hamas ndio upande pekee ambao bado hawajakubaliana na pendekezo la Rais Joe Biden la kusitisha mapigano, ambalo Washington inasema Israel tayari imekubali.

Rais al-Sisi amesisitiza umuhimu wa kuondoa vikwazo katika masuala ya kibinaadamu na msaada kwa wananchi wa Gaza.

Kabla ya ziara hii, mapigano makali yaliongeza ugumu kwenye juhudi za majaribio yote ya awali ya kukomesha mapigano, huku Israeli ikiendelea na mashambulio katikati na kusini mwa Ukanda wa Gaza.