Betancourt
3 Julai 2008Matangazo
BOGOTA:
Mwanasiasa wa Columbia Ingrid Bentacourt amewasili mji mkuu wa Columbia Bogota, pamoja na mateka wengine 14 waliokombolewa na majeshi ya Columbia.
Bentacourt na mateka hao wengine , ikiwa pamoja na wamarekani watatu walitekwa nyara na waasi wa Columbia wanaoitwa FARC.
Mwanasiasa huyo maaruf aliewahi kugombea urais wa nchi yake alitekwa nyara na waasi hao miaka zaidi ya sita iliyopita.
Mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kijeshi wa Bogota Bentacourt ambae pia ni raia wa Ufaransa alilakiwa na mama yake na ndugu zake wengine kadhaa.