1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mto Rhine wajaa maji

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaO

Mvua kubwa hapa Ujerumani zimesababisha kina cha mto Rhine kuzidi katika maeneo ya kusini magharibi.Usafiri wa maji umepigwa marufuku baada ya maji ya Mto huo kuongezeka sana kwa mujibu wa msemaji wa polisi mjini Karlsruhe bwana Rheinhold Seene.

Mtu mmoja anaripotiwa kuzama mjini Arnsberg baada ya kunasa kwenye sela baada ya maji kujaa.Kina cha mto Rhine kinatarajiwa kufikia futi 27 japo si cha juu zaidi kuripotiwa karne hii.