Benitez arejesha kumbukumbu Liverpool
26 Desemba 2018Liverpool ya Klopp imetengeneza mwanya wa pointi nne juu ya msimamo wa ligi wakati Benitez , meneja wa klabu hiyo kati ya mwaka 2004 na 2010 , anafanya ziara pamoja na timu yake ya Newcastle ambayo imo katika hatari ya kushuka daraja leo Jumatano (26.12.2012).
Kuna hisia nzito kwamba huu unaweza kuwa msimu ambao taji hilo la ligi ya England linaweza kuja Anfield kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990, licha ya kuwa historia ya hivi karibuni inatoa ujumbe mchanganyiko juu ya iwapo hicho kinaweza kutokea.
Kwanza, habari nzuri kwa Liverpool: Katika misimu minane kati ya 10 iliyopita, viongozi katika siku ya Krismasi wameweza kulinyakua taji hilo la ligi ya Premeier.
Na sasa habari mbaya: Katika mara mbili haikutokea, viongozi wa wakati wa sikukuu ya Krismasi walikuwa Liverpool.Katika mwaka 2008/09, Manchester United ilishinda ubingwa , katika mwaka 2013/14 ilikuwa Manchester City.
Kuanguka kwa wakati huo na kushindwa kupata ubingwa mwaka 2014 huenda ilikuwa maumivu ya hivi karibuni zaidi kwa mashabiki wa Liverpool , lakini kushindwa mwaka 2009, chini ya Benitez, huenda kunatoa sababu zaidi za kukata tamaa. Hali zote zinatoa masomo kwamba klabu hiyo ya Merseyside , hata hivyo, inaonekana klabu hiyo imeweza kuyamudu mambo hayo.
Kikosi cha Brendan Rodgers cha mwaka 2013 /14 hakikuwa na uwiano kama kikosi cha sasa cha kocha Klopp.
Wakati Rodgers alikuwa na safu ya ushambuliaji , ya Luis Suarez akisaidiwa na Daniel Sturridge ambaye yuko fiti, kikosi hicho kwa upande wa ulinzi ilikuwa na wasi wasi.
Meneja huyo wa Liverpool alikuwa na walinzi wanne , Martin Skrtel, Daniel Agger, Mamadou Sakho na Kolo Toure, lakini alisumbuka kupata wachezaji wawili wa kwanza. Timu iliyofunga mabao 101 ya ligi na kufungwa mabao 50, ni mengi mno kwa kikosi hicho kuweza kuwania kupata ubingwa.
Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe