Beckenbauer: Schweinsteiger apewe unahodha | Michezo | DW | 04.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Beckenbauer: Schweinsteiger apewe unahodha

Ni nani anayepaswa kutwikwa jukumu la kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Soka ya Ujerumani? Gwiji wa soka Ujerumani Franz Beckenbauer amependekeza kuwa Bastian Schweinsteiger anatosha kujaza pengo hilo

Nguli huyo wa soka la Ujerumani anasema Schwinsteiger wa Bayern Munich, ndiye aliye na sifa zinazoweza kumpa fursa ya kumrithi Philipp Lahm kama nahodha wa kikosi cha Die Mannschaft.

Beckenbauer ameliambia gazeti la maarufu la Ujerumani – Bild, kuwa Schweinsteiger ndiye kimantiki anayestahili kumrithi Lahm. Kwa sababu ana sifa za kuwa kiongozi, na alipata heshima kubwa kutokana na mchezo wake katika fainali ya Kombe la Dunia nchini Brazil.

Na mchezaji wa aina hiyo anaweza kuiinua timu. Inakuwa rahisi kwake kwa sababu alikuwa naibu wa Lahm kwa hivyo anafahamu majukumu anayostahili kuyatekeleza.

Beckenbauer anasema beki wa Borussia Dortmund Mats Hummels anastahili kuwa naibu wa Schweinsteiger badala ya kipa Manuel Neuer.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Rueters/APE
Mhariri: Mohammed Khelef