1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Bauhaus

Shule ya sanaa ya Bauhaus kutoka Ujerumani ilikuwa na athari kubwa siyo tu kwa tasnia ya usanifu majengo, lakini pia sanaa, ubunifu na nyanja nyingine. Inahusishwa kwa karibu sana na uwiano wa usanifu.

Bauhaus, ambacho kinafasiriwa kimsingi kama "nyumba ya ujenzi" iliasisiwa na Walter Gropius katika jamhuri ya Weimer mnamo mwaka 1919. Utulivu na kutokuwepo kwa mapambo vilikuwa muhimu katika shule ya Bauhaus. Ilihamia Dassau mwaka 1932 na mjini Berlin mnamo 1935 na pia iliendeshwa na Hannes Meyer na Ludwig Mies van der Rohe. Ubunifu ulioibuliwa na Bauhaus ulikuwa na ushawishi mkubwa hasa katika mataifa ya Marekani na Canada, na pia Israel. Mjini Tel Aviv, mkusanyiko wa majengo 4,000 ya Bauhaus umetambuliwa kuwa turaathi ya dunia ya Umoja wa Mataifa.