BASRA:Waingereza watatu wauawa Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 20.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BASRA:Waingereza watatu wauawa Iraq

Wizara ya ulinzi ya Uingereza imesema kuwa askari wake watatu wameuawa katika shambulio la kombora huko Basra nchini Iraq

Vifo hivyo vinafanya idadi ya askari wa Uingereza waliyouawa toka Marekani na majeshi ya washirika yalipoivamia Iraq kufikia 162.

Mjini Baghdad askari wawili wa Marekani wameuawa kutokana na shambulizi la bomu lililotegwa barabarani.

Lakini jeshi la Marekani limesema kuwa limefanikiwa kuwaua wanamgambo watatu na kuwakamata wengine 41.

Wakati huo huo Balozi wa Marekani nchini Iraq amewaambia wabunge wa Marekani kuwa kuna maendeleo ya kisiasa yaliyofikiwa nchini Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com