Basi la Hertha Berlin lafyatuliwa risasi | Michezo | DW | 10.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Basi la Hertha Berlin lafyatuliwa risasi

Basi la timu ya Hertha Berlin limefyatuliwa risasi jana siku moja tu kabla ya timu hiyo ya Bundesliga kupambana na Arminia Bielefeld katika mchuano wa Kombe la Shirikisho la Ujerumani – DFB Pokal

Hata hivyo basi hilo halikuwa na wachezaji wakati wa tukio hilo na dereva alinusurika bila majeraha yoyote. Dereva alikuwa akielekea kutoka hotelini kwenda kwenye kituo cha treni ili kuichukua timu wakati ambapo mtu aliyekuwa akiendesha pikipiki alipolifyatulia dirisha la mbele risasi.

Tukio hilo liliigubika michuano ya duru ya kwanza ambapo Bayern Munich waliwazaba Noettingen timu ya daraja la tano magoli matatu kwa moja wakati mahasimu wao wa Bundesliga Hamburg wakianguka katika kiunzi cha kwanza kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kufungwa magoli matatu kwa mawili katika muda wa ziada na timu ya daraja la nne Carl Zeiss Jena.

Hoffenheim ilishindwa mbili mtungi na klabu ya daraja la pili Munich 1860. Mabingwa watetezi Wolfsburg walipata ushindi wa magoli manne kwa moja dhidi ya Stuttgarter kickers wakati Borussia Dortmund wakishinda mbili sifuri dhidi ya Chemnitzer FC. Hanover na Mainz pian zilishinda mechi zao. Hii leo St Pauli itapambana na Borussia Moenchengladbach

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef