Bangkok | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Bangkok

Serikali yatishia kuwakamata na kuwatoza faini wafuasi wa upande wa upinzani

Bankok

Mvutano kati ya wafuasi wa serikali na wapinzani wao yanatishia kuzidi makali.Wafuasi 20 elfu wa chama tawala cha PPP wameandamana hii leo dhidi ya wapinzani wa chama cha "Muungano kwaajili ya demokrasia -PAD.Wanatishia kuivamia mahakama ya katiba iliyoamua jumanne iliyopita kuhusu uwezekano wa kuvunjwa chama cha PPP kutokana na udanganyifu uliofanyika wakati wa uchaguzi wa bunge mwaka mmoja uliopita.Leo asubuhi watu 50 walijeruhiwa guruneti liliporipuliwa karibu na makao makuu ya serikali.Wafuasi wa upande wa upinzani wa PAD wanaendelea kuvikalia viwanja vyote viwili vya ndege mjini Bankok.Baada ya njama ya kuyavamia majengo hayo kushindwa jana,serikali inatishia hivi sasa kuwafunga na kuwatoza faini wale wote watakaodharau sheria ya hali ya hatari.

 • Tarehe 30.11.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G6JN
 • Tarehe 30.11.2008
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G6JN
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com