Baibui linavyopoteza maana yake | Masuala ya Jamii | DW | 27.08.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Baibui linavyopoteza maana yake

Wakati ulimwengu ukibadilika, jamii za Waswahili hazikuachwa nyuma kwenye mabadiliko hayo, ambapo miongoni mwa mengi yaliyobadilika ni vazi la Baibui kwenye pwani ya Afrika Mashariki.

Mwanamke wa Kiswahili akiwa amevaa baibui la ukaja ama baibui la jadi ya Mswahili.

Mwanamke wa Kiswahili akiwa amevaa baibui la ukaja ama baibui la jadi ya Mswahili.

Ni bahati mbaya sana kwamba jamii hujikuza zikilazimika kuachilia tamaduni na mila zake kupotea, mambo ambayo ni muhimu sana kwa utambulisho wake kama jamii fulani. Katika makala hii ya Utamaduni na Sanaa, Amina Abubakar anaangazia kwa undani zaidi vazi lililotumiwa sana na wanawake wa Kiswahili kujistiri, buibui la ukaja au buibui la jadi la Kiswahili kama linavyojulikana na wengi.

Swali kubwa analouliza kwenye makala hii ni iwapo kutekwa kwake na mabuibui ya kisasa ni sawa na kuutupa utamaduni wa Kiswahili au muonekano wa asili ya mwanamke wa Kiswahili!

Kusikiliza makala nzima, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Amina Abubakar
Mhariri: Mohammed Khelef

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com