BAGHDAD.Watu 20 wameuwawa nchini Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 06.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD.Watu 20 wameuwawa nchini Irak

Takriban watu 20 wameuwawa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika mji wa Ramadi ulio kilomita 110 magharibi mwa mji mkuu wa Baghdad nchini Irak.

Taarifa ya polisi imearifu kuwa mlipuaji huyo wa kujitoa muhanga alijilipua ndani ya gari alilokuwa akiendesha.

Wato 30 wamejeruhiwa katika mlipuko huo ambao umesambaza gesi ya Chlorine.

Mapema leo mwandishi wa habari wa kituo cha radio cha Free Europe kinacho fadhiliwa na Marekani alipatikana amekufa.

Mwanamke huyo alikuwa na jeraha la risasi kichwani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com