BAGHDAD:Polisi wagundua miili iliyokatwa vichwa | Habari za Ulimwengu | DW | 28.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Polisi wagundua miili iliyokatwa vichwa

Polisi nchini Irak wamegundua miili 20 iliyokatwa vichwa amabyo ilikuwa imetupwa katika ufuo wa mto Tigris kusini mwa Baghdad.

Maiti hizo zote zilikuwa za wanaume ambao wanakisiwa kuwa na miaka kati ya 20 na 40. Hadi sasa miili bado haijatambuliwa.

Habari zaidi zinafahamisha kwamba kufuatia shambulio la bomu la leo asubuhi na ambalo limewauwa zaidi ya watu ishirini na mbili, katika kituo cha basi, polisi wametowa taarifa kwamba huwenda idadi ya watu waliokufa ikaongezeka.

Wahanga wa shambulio hilo la bomu walikuwa wansubiri usafiri katika kitongoji cha Bayaa kinachokaliwa na jamii kubwa ya Kishia.

Wakati huo huo wanajeshi watatu wa Uingereza waliuwawa katika shambulio jingine la bomu la kutegwa kando ya barabara katika mji wa Basra kusini mwa Baghdad, mwanajeshi wa nne alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com