BAGHDAD:Mauaji yaendelea Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 28.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

BAGHDAD:Mauaji yaendelea Iraq

Umwagikaji wa damu unaendelea huko Iraq hii leo wafanyikazi wane wa mashirika ya kutoa misaada wa shirika la hilali nyekundu wameuwawa na wengine watatu kujeruhiwa.

Mtu aliyekuwa na bunduki alivamia basi dogo katika eneo linalokaliwa na washia na wasunni katika mji wa Baddad na kuwashambulia abiria waliokuwemo ndani.

Watu wengine sita wameuwawa kwenye mashambulio matatu tofauti kusini mwa Baghdad.Katika tukio moja kundi la watu wakuzoa takataka lilishambuliwa na bomu la kutegwa kando ya barabara ambapo mtu mmoja aliuwawa na wanane wakajeruhiwa.

Katika kisa kingine watu wasiojulikana waliwauwa kwa kuwapiga risasi watu watano huko huko Baghdad.

Licha ya kufanyika opresheni kali ya kuweka usalama kwenye mji huo na wanajeshi wa Marekani na Iraq mashambulio ya wapiaganaji yanaendelea kushuhudiwa kwenye mji huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com