1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGDHAD: Mabomu yaua watu nchini Iraq

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2w

Kiasi watu ishirini na wawili wamefariki na wengine kama ishirini wamejeruhiwa baada ya mabomu mawili yaliyotegwa kwenye magari kulipuka kwenye vizuizi vya polisi karibu na madaraja mawili mjini Baghdad.

Kwa mujibu wa polisi madaraja hayo mawili yaliharibiwa kabisa baada ya milipuko hiyo iliyopishana kwa dakika chache.

Mashambulio hayo yametokea huku Marekani ikijitahidi kuwasaka wanamgambo wanaohusika na mabomu ya kujitoa mhanga mjini humo.

Hapo awali, majeshi ya Marekani yalisema yamefanya misako kadha kukabiliana na wanaohusika na mabomu yanayotegwa kwenye magari kote nchini Iraq na wakawaua wanamgambo wanne na wakawatia nguvuni wanamgambo wengine tisa.