1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bafana Bafana yajiwinda kunyakua taji la Afcon

Admin.WagnerD17 Januari 2015

Baada ya miaka kadhaa ya matokeo yasiyo na matumaini, Timu ya Taifa ya Afrika Kusini Bafanabafana inakwenda katika fainali za michuano ya kuwania kombe la Afrika la mataifa kwa kujiamini.

https://p.dw.com/p/1ELsN
Beerdigung von Senzo Meyiwa
Picha: Reuters

Wakati ikiweka matumaini hayo bado inakumbuka msimu mbaya uliomalizika mwaka 2014 kutokana na kifo cha nahodha na mlinda mlango wa timu hiyo Senzo Meyiwa, ambae aliuwawa katika tukio la ujambazi mwezi Oktoba.

Hivi sasa ikiwa ni sura tofauti kwa mabingwa wa wa Kombe la mataifa ya Afrika1996 chini ya kocha mpya Anatikisa Mashaba. Bfana Bafana hawajapoteza nafasi katika michezo 11 na wanajiamini kabla ya mashindano yatakayoanza huko Guinea ya Ikweta Jumamosi ijayo Januari 17.


‘Mwaka wa 1996 tulionesha kiwango kuwa sisi ni timu ya kuwa bingwa na ya ushindani'Mashaba aliwaambia waandishi wa habari mjini Johannesburg kabla ya timu kuondoka kwenda mashindanoni.

Kwenye timu tunajaribu kufufa moyo wa ushindani na kuonesha kuwa ni moja kati ya zile timu bora.

Bafana Bafana (Vijana, Vijana) kama ambavyo timu hiyo inajulikana, itaanza mashindano kwenye kundi C kwa mchezo wake dhidi ya Algeria timu iliorodheshwa kuwa namba moja Afrika- pambano litakalofanyika kwenye mji wa Mongomo siku ya Jumatatu, Januari 19.

Südafrika Fußball Nationalmannschaft
Kikosi cha timu ya taifa la Africa KusiniPicha: P. Utomi Epkei/AFP/Getty Images

Mechi nyingine za kundi hilo ni dhidi ya Senegal tarehe 23 Januari na Ghana tarehe 27 Januari kwenye kile kinachoonekana kama kundi la kifo.

David Minchela, mwandishi wa habari kutoka gazeti la michezo linalongoza Afrika Kusini -Laduma, anaamini kuwa matamshi ya kujiaamini kupindukia kutoka kwa kocha Mashaba yametowa mtihani kubwa kwa wachezaji.


‘Hatujawahi kuwa na timu bora na ngumu kwa hiyo kuweka matarajio makubwa ya namna hiyo kwenye timu, naamini Kocha ataifanya Bafana ianguke' alisema Minchela.


"Tutaondolewa mashindanoni kwenye raundi ya kwanza – Samahani kwa kusema hili,Urahisi wa kufaulu ni kama ndoto za alfajiri" Afrika Kusini haijawahi kukabiliana na shinikizo tokea walipoanza kushinda mchezo wao wa kwanza, aliongeza Minchella."Tukikutana na upinzani, huwa tunaporomoka“.


Bafana wameshindwa kufanya vizuri tokea waliposhinda AFCON 1996, licha ya kuwa moja kati ya timu inayopewa rasili mali za kutosha Afrika. Kwa sasa wako nafasi ya 51 kwenye orodha ya timu bora duniani.

Senzo Meyiwa Torhüter Torwart Südafrika
Nahonda na Kipa Senzo Meyiwa enzi za uhai wakePicha: Getty Images/Carl Fourie/Gallo Images

Mauaji ya nahodha na kipa Senzo Meyiwa na majambazi mwishoni mwaka jana jijini Johannesburg na ushauri wa nguvu kutoka kwa Mashaba kunaonekana kuiimarisha timu.


Kipa Meyiwa alipigwa risasi mbele ya mpenzi wake wakati wawili hao wakiingia kwenye nyumba moja katika kitongoji cha jiji hilo la Johannesburg karibu saa 2 usiku Oktoba 26.


Kocha Mashaba mwenye umri wa miaka 63, aliyechukua nafasi ya Gordon Igesund Julai mwaka jana, amewahi kuifundisha Bafana kati ya 2002 hadi 2004.


Maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Bafana yalianza Januari na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa wa zamani wa Afrika Zambia katika mechi iliyochzwa Johannesburg.


Jumapili iliopita , walitoka sare 1-1 na Cameroon kwenye mechi nyingine ya kujipima nguvu.


Wachezaji wengi wakiwamo mshambulizi Bernard Parker, viungo Thuso Phala, Sibusiso Vilakazi and Bongani Zungu wameonesha viwango vya juu wakati Mashaba akijaribu mbinu tofauti.

Mwandishi:Nyamiti Kayora/DPAE

Mhariri:Mohamed Abdul-Rahman