Arsenal yasaka kombe la FA | Michezo | DW | 22.05.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Arsenal yasaka kombe la FA

Arsenal yakosa nafasi  katika  Champions League  msimu ujao .. lakini inapigana  kumaliza vyema  msimu huu  kwa kunyakua kombe  la  FA dhidi  ya  Chelsea

Italien Neapel v Real Madrid - UEFA Champions League Robert Lewandowski (picture alliance/empics/J. Walton)

Laurent Koscielny wa Arsenal (kulia akipambana na Robert Lewandowski wa Bayern Munich

Arsenal London  iko  katika  nafasi  nzuri  ya  kuibuka washindi  wa  kombe  la  FA  nchini  Uingereza  kwa kuiangusha  Chelsea  katika  fainali  kwa  kuwa wanahamasa  ya  juu  kumaliza  msimu  huu  kwa mafanikio  baada  ya  kushindwa  kufuzu  kucheza  katika Champions League, amesema   kocha  wa  mabingwa  wa ligi  ya  Uingereza , Premier League  Chelsea  Antonio Conte.

UEFA EURO 2016 Italien vs Irland +++ Trainer Conte verzweifelt (Reuters/G. Fuentes)

Kocha wa Chelsea Antonio Conte

Chelsea  walianza  sherehe za  ubingwa  baada  ya kuishinda  Sunderland  kwa  mabao 5-1 siku  ya  Jumapili na  wanaweza  kushinda  vikombe  viwili  vya  nyumbani kwa  kuishinda  Arsenal, ambao  wameshindwa  kuingia katika  timu  nne  bora za  ligi  hiyo  licha  ya  kushinda kwa mabao 3-1 dhidi  ya  Everton jana  Jumapili.

Conte anaweza  kuwa  kocha  wa  pili kushinda  mataji mawili  katika  msimu  wake  wa  kwanza  baada  ya Mtaliani  mwenzake Carlo Anceloti kufanya  hivyo katika msimu  wa  2009-10. Real madrid  nao  wametawazwa mabingwa  wa  La Liga  nchini  Uhispania , na  kuivua  taji hilo Barcelona  kwa  mara  ya  kwanza  katika  muda  wa miaka  5, na  hili  ni  taji  lao la  33. Nao Juventus  Turin imefanikiwa  kwa  mara  ya  6  mfululizo  kuwa  mabingwa wa  Italia. AS Monaco wametawazwa  mabingwa  wa  ligi ya Ufaransa Leage 1 kwa  mara  ya  kwanza  tangu  mwaka 2000.

Italien Juventus Turin vorzeitig italienischer Meister (Getty Images/AFP/F. Monteforte)

Juventus Turin wakishangiria ubingwa wao wa sita mfululizo katika ligi ya Italia Serie A

Manchester United  na  Ajax Amsterdam zinakutana  katika fainali  ya  kombe  la  Ulaya  siku  ya  Jumatano katika pambano  la  vigogo  wa  zamani  wa  bara  hili. Ajax na Manchester  United  zina  nafasi  ya  kulinyakua  taji  la  ligi ya Ulaya  siku  ya  Jumatano wakati  timu  zote  zina  lengo la  kupiga  hatua  nyingine  kurejea  katika medani  ya vigogo vya  soka la  Ulaya. Kwa Ajax mabingwa  mara  nne wa  Ulaya , mchezo  huo  wa  fainali mjini  Stockholm ni  wa kwanza  katika  bara  la Ulaya  tangu  mwaka 1996, wakati walipopoteza  ubingwa  wa  Champions league kwa mikwaju  ya  penalti.

Fußball Europa-League Ajax Amsterdam vs. Olympique Lyon (Reuters/M. Kooren Livepic)

Wachezaji wa Ajax Amsterdam katika kombe la ligi ya Ulaya wanapambana na Manchester United

United itakuwa  katika  fainali  ya  Ulaya  tangu  mwaka 2011  ambapo  ilipoteza  fainali  ya  Champions League dhidi  ya  Barcelona , na  kwa  hakika  inanafasi  nzuri kuliko  wapinzani  wao.

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo

Mhariri: Mohammed Khelef

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com