1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Arsenal yaongoza nane bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya

29 Januari 2026

Arsenal imekuwa timu ya kwanza kushinda mechi zote nane kwenye hatua ya ligi ya michuano ya Mabingwa Ulaya kufuatia ushindi wa 3-2 dhidi ya Kairat Almaty ya Kazakhstan Jumatano usiku.

https://p.dw.com/p/57eOQ
Soka Champions League | FC Bayern Munich dhidi ya Bayer 04 Leverkusen
Bayer 04 Leverkusen katika uwanja wa Allianz Arena, Munich, Champions League, Robo fainali 05.03.25Picha: picture alliance / HMB Media

Kocha wa Arsenal ambayo kwa sasa inashika usukani Mikel Arteta amesifu kiwango cha kikosi chake walichoonyesha kwenye hatua hii ya awali ya michuano hiyo.

Kairat inayoshiriki kwa mara ya kwanza imemaliza ikiwa nafasi ya mwisho kwenye orodha ya timu 36 ikiwa na pointi moja tu, baada ya mechi hizo nane.

Kwa upande mwingine, mshambuliaji wa Real Madrid, Kylian Mbappe amekiri kwamba timu yake haikuwa katika nafasi nzuri, na kushindwa kuingia kwenye nane bora, baada ya kichapo cha 4-2 dhidi ya Benfica ya Jose Mourinho.

Madrid mabingwa mara 15 wa Champions, sasa watalazimika kucheza mechi ya kufuzu ili kusonga mbele.