Arsenal yaisambaratisha Chelsea | Michezo | DW | 28.12.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Arsenal yaisambaratisha Chelsea

Chelsea jana ilichapwa mabao 3-1 na Arsenal na hivyo kuzidi kupoteza matumaini ya kutetea ubingwa wao wa ligi kuu ya Uingereza.

Kocha wa Arsena Arsene Wenger

Kocha wa Arsena Arsene Wenger

Yalikuwa ni mabao ya Alex Song, Cesc Fabregas na Theo Walcott yaliyopeleka majonzi Stamford Bridge.

Arsenal sasa imefikisha pointi 35, nyuma ya vinara Manchester United wenye pointi 37, huku Chelsea ikibakia katika nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 31.

Kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti alikiri kuwa hali si nzuri kwao, na kwamba ni lazima waamke, ingawaje hana wasiwasi.

Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters

Mhariri:Josephat Charo