Appiah atimuliwa kama kocha wa Ghana | Michezo | DW | 13.09.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Appiah atimuliwa kama kocha wa Ghana

Shirikisho la kandanda nchini Ghana limethibitisha kuwa limemtimua kocha wa timu ya taifa Kwesi Appiah, na kumaliza miezi ya uvumi kuhusiana na hatima ya kocha huyo mwenye utata.

Tangazo hilo limekuja baada ya matokeo mabaya ya Ghana katika dimba la mwaka huu la Kombe la Dunia nchini Brazil ambapo Black Stars walishindwa kujiondoa katika kundi lao.

Tangazo la kufutwa kazi Appiah limekuja saa 48 baada ya ushindi wao ugenini dhidi ya Togo kuifufua kampeni yao ya kufuzu katika dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika.

Ghana iliifunga Togo mabao matatu kwa mawili katika mechi ya mwisho ya Kundi E Jumatano wiki hii baada ya kuwa na mwanzo mbaya mwishoni mwa wiki iliyopita wakati walipokabwa kwa sare ya goli moja kwa moja na Uganda mjini Kumasi.

Duru nchini humo zinasema kuwa Mserbia Milovan Rajevic, kocha wa zamani wa Black Stars kuanzia mwaka wa 2008 hadi 2010, huenda akarejea usukani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/AP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman